• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 13, 2020

  CORONA; ENGLAND YASITISHA MECHI ZOTE ZA SOKA HADI APRILI 3

  MECHI za Ligi kuu ya soka ya England zitaahirishwa hadi Aprili 3 angalau kufuatia baadhi ya wachezaji wa ligi hio kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona.
  Mechi za mashindano yote kuanzia Ligi ya Mabingwa Ulaya, UEFA Europa League, Ligi Kuu ya England na za chini hadi za wanawake ambazo zilitarajiwa kuchezwa wiki ijayo, zimeahirishwa kutokana na mlipuko wa coronavirus.
  Droo kwa ajili ya raundi ijayo, iliyopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, pia imeahirishwa.
  Katika Ligi ya Mabingwa, mechi kati ya Manchester City dhidi ya Real Madrid, Juventus dhidi ya Lyon, Barcelona dhidi ya Napoli na Bayern Munich dhidi ya Chelsea zote zimeahirishwa.

  Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa.
  Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na 18 Machi pia zimesitishwa.
  Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatolewa baadae".
  Bodi ya Soka ya Ulaya imewaalika wawakili wa wajumbe wa mashirikisho yote 55 kwa mkutano siku ya JUmanne ili kujadili mkakati wa kukabiliana na mlipuko wa coronavirus.
  Mechi za Manchester United, Wolves na Rangers katika Ligi ya Ulaya pia zimefutwa.
  Mechi zote za robo fainali ya Ligi ya Ulaya ya vijana zilizokuwa zimepangwa kuchezwa tarehe 17 na18 Machi pia zimesitishwa.
  Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatolewa baadae".
  Bodi ya Soka ya Ulaya imewaalika wawakili wa wajumbe wa mashirikisho yote 55 kwa mkutano siku ya Jumanne ili kujadili mkakati wa kukabiliana na mlipuko wa coronavirus.
  Uefa imesema kuwa maamuzi saidi kuhusu mpangilio wa kuahirisha mechi hizo "yatatolewa baadae". Mpangilio wa Euro 2020 utajadiliwa katika mkutano huo.
  Zaidi ya watu 125,000 wamepatikana na virusi vya corona katika nchi 118 kote duniani, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO. Idadi kamili ya vifo vya watu ni zaidi ya 4,600.
  Mechi zilizoahirishwa zilizotarajiwa kuchezwa kati ya Machi 17 hadi 19 kuanzia Ligi ya Mabingwa: Bayern Munich dhidi ya Chelsea, Barcelona dhidi ya Napoli, Manchester City dhidi ya Real Madrid na Juventus dhidi ya Lyon.
  Europa League; Bayer Leverkusen dhidi ya Rangers, Getafe dhidi ya Inter Milan, Shakhtar Donetsk dhidi ya Wolfsburg, Wolves dhidi ya Olympiakos, FC Basel dhidi ya Eintracht Frankfurt, FC Copenhagen dhidi ya Istanbul Basaksehir na Manchester United dhidi ya LASK.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CORONA; ENGLAND YASITISHA MECHI ZOTE ZA SOKA HADI APRILI 3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top