• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 14, 2020

  POLISI TANZANIA YAICHAPA NDANDA FC 1-0 MOSHI, SINGIDA UNITED WAITANDIKA MBEYA CITY 2-1

  Na Mwandishi Wetu, KILIMANAJRO
  TIMU ya Polisi Tanzania imeibuka na ushind wa 1-0 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Kwa ushindi huo uliotokana na bao la penalti la Marcel Boniventure Kaheza dakika ya 13, Polisi Tanzania iliyopanda Ligi Kuu msimu huu inafikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 29 na kusogea nafasi ya sita nyuma ya Coastal Union yenye pointi 46 za mechi 28.
  Mechi nyingne za Ligi Kuu, Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli FC, bao pekee la Abdul Swamadi dakika ya 78.
  Nayo Singida United imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Liti, zamani Namfua mkoani Singida. Mabao ya Singida United yamefungwa na Erick Mambo dakika ya 71 na Elinywesia Sumbi dakika ya 81, wakati la Mbeya City limefungwa na Mohamed Kapeta dakika ya 15.
  Mwadui FC imeichapa Tanzania Prisons ya Mbeya pia, mabao 2-1 Uwanja wa Mwadui Complex, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Wallace Kiango dakika ya 12 na Raphael Aloba dakika ya 83 huku la Prisons likifungwa na Samson Mbangula dakika ya 90 na ushei.
  Bao la dakika ya 79 la Jaffary Salum Kibaya limeinusuru Mtibwa Sugar kulala nyumbani, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United iliyotangulia kwa bao la Ramadhan Chombo ‘Redondo’ dakika ya 45 na ushei Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro. 
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi mbili, Namungo FC wakiikaribisha Yanga SC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi na KMC wakiwa wenyeji wa Alliance Uwanja wa Uhuru kuanzia Saa 10:00 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YAICHAPA NDANDA FC 1-0 MOSHI, SINGIDA UNITED WAITANDIKA MBEYA CITY 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top