• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 05, 2020

  KMC YAZINDUKA NA KUICHAPA JKT TANZANIA 1-0, MWADUI FC NAYO YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya KMC imezinduka baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania asubuh ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Mchezo huo ulishindikana kufanyika jana kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na leo shujaa akaibuka kiungo Mohamed Ally Samatta aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 17.
  Katika mchezo huo, JKT Tanzania walipata bao lililofungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 19, hata hivyo likakataliwa mfungaji akidaiwa alikuwa ameotea.
  Nayo Lipuli FC ikalazimishwa sare ya 3-3 na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Samora mjini Iringa. Mabao ya Lipuli yamefungwa na Paul Nonga dakika ya 14 na 72 na Frank Sekule dakika ya 52, wakati ya Ndanda yamefungwa na Omary Ramadhani dakika ya 22 Vitalis Mayanga dakika ya 48 na 88. 
  Mwadui FC ikaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga, mabao yake yakifungwa na Abubakar Kambi dakika ya 27 na Gerrald Mathias dakika ya 90 na ushei, huku la wageni likifungwa na Marcel Kaheza dakika ya 61.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KMC YAZINDUKA NA KUICHAPA JKT TANZANIA 1-0, MWADUI FC NAYO YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top