• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 07, 2020

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-1 GAIRO, KMC NAYO YAIPIGA MBAO FC 2-0 UHURU

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  TIMU ya Mtibwa Sugar leo imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya ndugu zao, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Juma Luizio dakika ya 16, Awadh Juma dakika ya 69 na  Jaffar Kibaya dakika ya 82, baada ya Kagera Sugar kutangulia kwa bao la Nassor Kapama dakika ya sita .
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 27 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 12.

  Nayo KMC FC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC, mabao ya Hassan Kabunda dakika ya nane na Abdul Hillary dakika ya 19, wakati bao pekee la Enock Mkanga dakika ya 26 likapa Mwadui FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mwadui Complex, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
  Singida United ikapoteza mechi nyngine nyumbani, baada ya kuchapwa 2-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa Liti. Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Samson Mangula dakika ya 17 na 29, wakati bao pekee la Singida limefungwa na Haruna Moshi ‘Boban’ dakika ya 45.
  Bao la penalti la Fully Maganga dakika ya 31 likaisaida Ruvu Shooting kupata sare ya 1-1 na JKT Tanzania iliyotangulia kwa bao la Hassan Mwaterema dakika ya 18, wakati Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya 0-0 na Namungo FC Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
  Nayo Coastal Union imelazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga leo.
  Mchana wa leo, bao pekee la Frank Raymond Domayo dakika ya 85 likaipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-1 GAIRO, KMC NAYO YAIPIGA MBAO FC 2-0 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top