• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 25, 2020

  MBWANA SAMATTA AONYESHA YEYE NI “CHIZI MABENZI” BAADA YA KUNUNUA BENZ YA TATU ULAYA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameonyesha yeye ni mpenzi mno wa gari aina ya Mercedes Benz.
  Akiwa katika mwezi wa pili tu tangu ajiunge na klabu yake mpya, Aston Villa nchini England, Nahodha huyo wa Taifa Stars, Samatta tayari amenunua gari mpya aina ya Mercedes Benz ya kisasa kabisa, kwa maana ya toleo jipya.
  Kwake hiyo inakuwa Mercedes Benz ya tatu tangu ahamie Ulaya Januari mwaka 2016 alipojiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Mbwana Samatta amenunua Mercedes Benz mpya na ya kisasa kabisa baada ya kutua England

  Katika miaka yake minne ya kuwa Genk, Samatta anayejulikana kama Captain Diego kwa jina la utani, amemiliki Mercedes Benz mbili, moja nyeusi iliyokuwa na namba za usajili 1- HRP - 835 na nyingine nyekundu, iliyokuwa na namba za usajili 1- HRP -853.
  Lakini pia akiwa Genk, Samatta aliyeuzwa kwa dau la Pauni Milioni 10 kwenda Aston Villa ya England – alimiliki pia gari aina ya Range Rover iliyokuwa na namba za usajili 1- VQE – 376.
  Na wakati akiwa Mazembe, Samatta pia alinunua Range Rover nyekundu ikiwa moja ya gari tatu alizowahi kumiliki akiwa na klabu hiyo ya Lubumbashi kati ya 2011 na 2016.
  Bado inakumbukwa gari ya kwanza ya Samatta mwenye umri wa miaka 27 sasa ni Toyota Mark II Grande/GF-GX100 aliyopewa baada ya kusajiliwa na klabu ya Simba SC mwaka 2010 akitokea African Lyon, zamani Mbagala Market, zote za Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBWANA SAMATTA AONYESHA YEYE NI “CHIZI MABENZI” BAADA YA KUNUNUA BENZ YA TATU ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top