• HABARI MPYA

  Thursday, March 12, 2020

  LIVERPOOL YAPIGWA 3-2 NA ATLETICO MADRID NA KUVULIWA TAJI LA ULAYA

  Wachezaji wa Liverpool wakisikitika baada ya kuvuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kufungwa 3-2 na Atletico Madrid jana Uwanja wa Anfield katika mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 kufuatia kuchapwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Jijini Madrid Februari 18.  
  Liverpool jana iltangulia kwa bao la Georginio Wijnaldum dakika ya 43 na kufanya sare ya jumla ya 1-1, hivyo mchezo ukahamia kwenye dakika za 30 za nyongeza, ambako wenyeji walitangulia tena kwa bao la Roberto Firmino dakika ya 94, kabla ya Atletico Madrid kuzinduka kwa mabao ya Marcos Llorente dakika ya 97 na 105 na Alvaro Morata dakika ya 120 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAPIGWA 3-2 NA ATLETICO MADRID NA KUVULIWA TAJI LA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top