• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 26, 2020

  SHANGHAI SHENHUA YAMPA IGHALO OFA YA MKATABA MPYA MNONO

  KLABU ya Shanghai Shenhua ya China imetoa ofa ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wake Odion Ighalo (30) ambaye anacheza kwa mkopo Manchester United.
  Mkataba wa sasa ulikuwa unamalizika mwaka 2022, lakini Shanghai baada ya kuridhika na kiwango chake cha hivi karibuni, wanataka kuendelea kumiliki Mnigeria huyo hadi mwaka 2024, kwa malipo ya paundi 400,000 kwa wiki.
  Kwa upande wake Ighalo anachusubiri ni ofa itakayotolewa na Man United baada ya mkopo wake kumalizika mwezi Juni mwaka huu kwani imekuwa ni ndoto yake ya maisha kukipiga kwa mashetani hao wekundu wa Jiji la Manchester.
  Shanghai Shenhua inataka Odion Ighalo arejee China kwa mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHANGHAI SHENHUA YAMPA IGHALO OFA YA MKATABA MPYA MNONO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top