• HABARI MPYA

    Saturday, February 02, 2019

    MTOTO WA AFIF WA SIMBA AIPA QATAR UBINGWA WA ASIA

    WINGA mwenye asili ya Tanzania, Akram Hassan Afif jana ameifungia timu ya taifa ya Qatar bao la tatu dakika ya 83 kwa penalti ikiichapa Japan 3-1 katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Asia Uwanja wa Zayed Sports City mjini Abu Dhabi.
    Kabla ya kufunga bao hilo, mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Simba SC, Hassan Yahya Afif, alitoa pasi za mabao yote mengine ya Qatar, la kwanza lililofungwa na Almoez Ali dakika ya 12 na la pili lililofungwa na  Abdulaziz Hatem dakika ya 27, wakati bao pekee la Japan lilifungwa na Takumi Minamino dakika ya 69.
    Akram mwenye umri wa miaka 22, anatambulishwa kama mwanasoka wa kimataifa wa Qatar mwenye asili ya Yemeni na Somalia kwa sababu ya wazazi wake ambao wamewahi kuishi Tanzania. 
    Wachezaji wa Qatar wakisherehekea na taji lao bao ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Asia Uwanja wa Zayed Sports City mjini Abu Dhabi jana 
    Akram Afif akishangilia baada ya kuifungia Qatar bao la tatu jana mjini Abu Dhabi 

    Alizaliwa Novemba 18, mwaka 1996 mjini Doha, Qatar miaka mitano tu tangu baba yake, Hassan Afif aisaidie Simba kutwaa la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati kabla ya kuhamia Uarabuni ambako anaishi hadi sasa.
    Kisoka aliibukia klabu ya Al Markhiya mwaka 2004 hadi 2006, ambayo aliwahi kuichezea hata kiungo wa zamani wa Simba, Mwinyi Kazimoto kabla ya kununuliwa kwa dau kubwa na Al Sadd mwaka 2006 na mwaka 2009 akachukuliwa katika akademi ya Aspire.
    Na akiwa huko akaivutia klabu ya Sevilla ya Hispania iliyomsajili kwa dau zuri mwaka 2012, kabla ya kumtoa kwa mkopo Al Sadd mwaka 2014 ambako anaendelea kucheza hadi sasa akipata uzoefu zaidi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTOTO WA AFIF WA SIMBA AIPA QATAR UBINGWA WA ASIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top