• HABARI MPYA

    Saturday, October 15, 2016

    MAVUGO AANZA KUZOESHWA MAISHA YA BENCHI SIMBA

    KWA mara ya pili mfululizo, kocha Mcameroon Joseph Marius Omog hajampanga mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.
    Simba SC inawakaribisha Kagera Sugar ya Bukoba katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kama ilivyokuwa Jumatano kwenye mechi na Mbeya City, Mavugo na leo yupo benchi.
    Laudit Mavugo ameanzishwa benchi na leo Simba ikimenyana na Kagera Sugar

    Kikosi kinachoanza Simba leo ni; Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Juuko Murshid, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Muzamil Yassin, Mwinyi Kazimoto, Frederic Blagnon, Ibrahim Hajibu na Shizza Kichuya. 
    Katike benchi wapo Peter Manyika, Abdi Banda, Jamal Mnyate, Mavugo, Novart Lufunga, Said Ndemla na Mohamed 'MO' Ibrahim.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAVUGO AANZA KUZOESHWA MAISHA YA BENCHI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top