• HABARI MPYA

  Sunday, October 23, 2016

  TOTO CHOVU LA YANGA LITAWEZA NINI KWA SIMBA HII ITAFUNAYO HADI MBAO?

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TOTO Africans inayoonekana dhaifu zaidi kwa katika miaka ya karibuni leo itakuwa mgeni wa Simba SC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Ikitoka kufungwa na ‘baba zao’ Yanga 2-0 katikati ya wiki Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Toto leo inakutana na timu bora zaidi katika Ligi Kuu hadi sasa msimu huu, Simba.
  Simba ndiyo inaongoza Ligi Kuu hadi sasa ikiwa imejikusanyia pointi 26 katika mechi 10, wakifuatiwa na mahasimu wao wa jadi, Yanga wenye pointi 21 za mechi 10 pia.
  Toto Africans inayoonekana dhaifu zaidi kwa katika miaka ya karibuni leo itakuwa mgeni wa Simba SC Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam 

  Toto ambayo imekuwa moja ya timu mbili zilizobadilisha makocha kwa matokeo mabaya, ikimfukuza Rogasian Kaijage na kumpa nafasi, Khalfan Ngassa ipo Dar es Salaam tangu juzi.
  Mwadui FC ya Shinyanga imeachana na Jamhuri Kihwelo na sasa iko mbioni kumchukua Salum Mayanga wa Mtibwa Sugar. 
  Hata hivyo, kocha wake mpya wa muda Ngassa amezuiwa na TFF kukaa kwenye benchi kwa madai hana vyeti vya kitaaluma – maana yake leo ataishia vyumbani.
  Kocha Mcameroon wa Simba SC, Joseph Marius Omog aliyeshinda kwa mbinde 1-0 mechi iliyopita dhidi ya Mbao FC ya Mwanza, ameshaweka wazi dhamira yake ya kutotaka kupoteza hata pointi moja katika mechi zote za Ligi Kuu. 
  Anataka kushinda mechi zote ili kujikusanyia mtaji wa kutosha wa pointi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu.  
  Kweli Toto imekuwa ikifahamika kama moja ya timu kiboko za Simba, lakini ya msimu huu inaonekana kuwa dhaifu, je leo itaweza kuendeleza rekodi yake?
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TOTO CHOVU LA YANGA LITAWEZA NINI KWA SIMBA HII ITAFUNAYO HADI MBAO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top