• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 30, 2016

  TAMBWE ANAANZA NA CHIRWA LEO YANGA DHIDI YA MBAO, NGOMA ANASUBIRI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya kutokea benchi Jumatano na kufunga mabao mawili, Yanga ikishinda 4-0 dhidi ya JKT Ruvu, mshambuliaji Mrundi Amissi Joselyn Tambwe leo ameanzishwa dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.
  Yanga inaikaribisha Mbao FC leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuuya Vodacom Tanzania Bara ikitoka kushinda 4-0 Jumatano dhidi ya JKT Ruvu, mabao mengine yakifungwa na Simon Msuva na Obrey Chirwa.
  Na Tambwe hajaanza tangu Jumatano ya Oktoba 12 Yanga ikishinda 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, siku ambayo alipasuka kwenye paji la uso baada ya kugongana na Nahodha na kiungo wa wapinzani, Shaaban Nditi mwishoni mwa mchezo.
  Amissi Tambwe (katikati) leo ameanzishwa Yanga dhidi ya Mbao FC ya Mwanza

  Kutoka hapo, Tambwe akakosa mechi mbili zilizofuata dhidi ya Azam FC Oktoba 16 timu hizo zikitoka sare ya 0-0 Uhuru na Oktoba 19 dhidi ya Toto Africans Yanga ikishinda 2-0 Uwanja wa Kirumba, Mwanza kabla ya kutokea benchi dakika za mwishoni kwenye mechi na Kagera Sugar Oktoba 22 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba timu yake ikishinda 6-2.
  Na baada ya Jumatano kutumia muda mfupi kufunga mabao mawili kwa jitihada binafsi, Tambwe leo ameanzishwa pamoja na Mzambia Obrey Chirwa katika safu ya ushambuliaji.
  Kwa ujumla kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Mbao FC ni; Deogratius Munishi 'Dida', Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke.
  Katike benchi wapo Benno Kakolanya, Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Donald Ngoma na Matheo Anthony.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TAMBWE ANAANZA NA CHIRWA LEO YANGA DHIDI YA MBAO, NGOMA ANASUBIRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top