• HABARI MPYA

  Monday, October 31, 2016

  MASHALI AUAWA AKIDHANIWA NI MWIZI KIMARA


  BONDIA Thomas Fabian Mashali amefariki dunia baada ya kupigwa na watu ambao bado hawajajulikana usiku wa kuamkia leo eneo la Kimara Bonyokwa, Dar es Salaam.
  Taarifa ambazo zimeifikia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE zinasema kwamba mwili wa mbabe huyo aliyezaliwa Septemba 9 mwaka 1989, kwa sasa upo hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuokotwa Tabata.
  Msiba wa bingwa huyo wa mataji ya WBO na UBO International upo nyumbani kwao, Tandale mjini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa bondia Cossmas Cheka ni kwamba Mashali ameuawa na wananchi waliodhani ni mwizi baada ya bondia huyo kwenda kudai fedha zake Kimara Bonyokwa.
  "Mashali tulikuwa naye kwenye kikao Musoma Bar (Temeke), baada ya kikao akatuaga akasema anakwenda kudai fedha zake Kimara. Sasa inasemekana katika kudaiana na hao jamaa ukatokea ugomvi,"alisema Cheka.
  Taarifa nyingijne zinasema wagomvi wa Mashali baada ya kuzidiwa katika ugomvi wakapiga kelele za mwizi na ndipo wananchi walipotokea na kumpiga hadi hali yake kuwa mbaya.
  Lakini baadaye wakatokea watu waliomfahamu bondia huyo na kumuokoa na kumpeleka hospitali ambako iligundulika amekwishafariki dunia. Taarifa ya Polisi bado inasubiriwa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHALI AUAWA AKIDHANIWA NI MWIZI KIMARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top