• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 24, 2016

  MAMELODI SUNDOWNS MABINGWA WAPYA WA AFRIKA

  TIMU ya Mamelodi Sundowns imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kipigo cha bao 1-0 usiku wa Jumapili kutoka kwa wenyeji Zamalek Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, Misri.
  'Wabrazil' wanavikwa Medali za Dhahabu za ubingwa wa Afrika kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya awali kushinda 3-0 nyumbani, Afrika Kusini.
  Timu hiyo ya Tshwane inakuwa ya pili kutoka Afrika Kusini kutwaa taji hilo la Afrika baada ya Orlando Pirates iliyobeba ubingwa huo mwaka 1995.
  Bao pekee la Zamalek leo limefungwa na Stanley Ohawuchi dakika ya 64 ambalo linaunganishwa kwenye matokeo ya wiki iliyopita Uwanja wa Lucas Moripe Stadium mjini Atteridgeville.
  Kikosi cha Zamaelek kilikuwa: Gennesh; Khaled/Shikabala dk76, Dweidar, Gabr, Youssef - Hamed/Salah dk85, Tawfik - Ohawuchi, Hefny/Mayuka dk85, Fathi - Morsy.
  Mamelodi Sundowns: Onyango/Sandilands dk28, Langerman, Nthethe, Soumahoro, Mbekile - Kekana, Mabunda - Dolly, Tau, Laffor/Modise dk72 - Billiat/S.Zwane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAMELODI SUNDOWNS MABINGWA WAPYA WA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top