• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 28, 2016

  KIPA NAMBA MOJA AREJEA MTIBWA

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  HABARI njema kwa mashabiki wa Mtibwa Sugar, kipa namba moja wa timu hiyo Said Mohammed Nduda amepona na sasa anapambana kurejea uwanjani.
  Mduda aliyekuwa nje ya Uwanja tangu mwanzoni mwa msimu juzi alianza mazoezi kikamilifu na wachezaji wenzake wakati timu ikijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Toto Africans Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 
  “Ninamshukuru Allah (Mungu) kwa kuniwezesha kupona tena na kurudi tena uwanjani. Jana (juzi) nimeanza mazoezi kikamilifu na wachezaji wenzangu,”alisema Ndunda.
  Kipa Said Mohammed Nduda akiwa amebebwa na wachezaji wenzake kabla ya kuumia

  Kipa huyo wa zamani wa Yanga na Maji Maji alisema kwamba ana hamu ya kurejea uwanjani kuisaidia timu yake baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu.
  Pamoja na hayo, Mduda aliwapongeza wachezaji wenzake kwa kuipigania vizuri tangu mwanzo mwa msimu hadi kuifanya iwe ndani ya tano bora kwenye msimamo wa Ligi Kuu. 
  “Timu ipo kwenye nafasi nzuri, ipo nafasi ya nne maana yake hata sisi tumo kwenye mbio za ubingwa. Kwa kwa kweli nawapongeza wachezaji wenzangu na benchi zima la ufundi, na mimi sasa naungana nao kuongeza nguvu,”alisema.
  Mtibwa Sugar inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa pointi zake 17 ilizokusanya kwenye mechi 12, ikishinda nne, sare tano na kufungwa tatu.
  Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 29 za mechi 11, ikifuiatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 24 za mechi 11 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPA NAMBA MOJA AREJEA MTIBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top