• HABARI MPYA

  Friday, October 28, 2016

  MAN UNITED YATEGESHEWA NYUNDO ROBO FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND

  Juan Mata alikuwa shujaa wa Manchester United dhidi ya mahasimu wao, Manchester City kwenye hatua ya 16 Bora

  RATIBA ROBO FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLANMD:

  Manchester United v West Ham
  Hull v Newcastle
  Liverpool v Leeds 
  Arsenal v Southampton 
  (Mechi zitachezwa Novemba 28, mwaka huu wakati Nusu Fainali mechi za kwanza zitakuwa Januari 9, marudiano Januari 23 na Fainali Februari 26 mwakani 
  BAADA ya kuwatoa mahasimu wao wa Jiji, Manchester City kwenye hatua ya 16 Bora, Manchester United watamenyana na West Ham Uwanja wa Old Trafford katika Robo Fainali ya Kombe la Ligi England.  
  Mechi nyingine itakayohusisha wapinzani wa Ligi Kuu ya England watupu, Arsenal itamenyana na Southampton Uwanja wa Emirates baada ya timu hizo kuzitoa Reading na Sunderland.
  Hull City walio katika msimu mgumu Ligi Kuu ya England, watakuwa nyumbani Uwanja wa KCOM kuwakaribisha vinara wa Daraja la Kwanza, maarufu kama Championship, Newcastle United.
  Na timu ya kocha Mjerumani, Jurgen Klopp itamenyana na Leeds katika raundi inayofuata Uwanja wa Anfield.  Mechi za Robo Fainali ya Kombe la Ligi zinatarajiwa kuchezwa Novemba 29 na 30.
  Mara ya mwisho United kucheza na West Ham kwenye Kombe la Ligi, Wagonga Nyundo wa London walishinda 4-0 mwaka 2010.
  United ililipa kisasi kwa mahasimu wao, Man City usiku wa Jumatano kwa ushindi wa 1-0, shukrani kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Hispania Juan Mata, wakati West Ham ilisonga mbele kwa kuifunga Chelsea 2-1 Uwanja wa London.
  Habari mbaya kwa mashabiki wa Arsenal kuelekea mchezo na Southampton, timu ya Arsene Wenger imepoteza mechi zake tatu mfululizo zilizopita nyumbani dhidi ya timu za Ligi Kuu. 
  Hull City haijawahi kufika Nusu Fainali ya michuano hiyo, wakati timu ya kocha Rafa Benitez, Newcastle mara ya mwisho ilifika hatua hiyo ya nne bora mwaka 1976.
  Mara mbili za mwisho Liverpool na Leeds zilipokutana kwenye michuano hiyo, ilikuwas Raundi ya Tatu, na Wekundu walishinda 1-0 Uwanja wa Elland Road, bao pekee la David N'gog mwaka 2009.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATEGESHEWA NYUNDO ROBO FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top