• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 25, 2016

  ATLETICO MADRID WATAWALA TUZO ZA LA LIGA, BARCA WASUSA...RONALDO APUUZWA!

  Nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa La Liga msimu wa 2015-16

  WASHINDI WA TUZO ZA LA LIGA MSIMU WA 2015-16 

  Mchezaji Bora: Antoine Griezmann (Atletico Madrid)
  Kocha bora: Diego Simeone (Atletico Madrid)
  Kipa Bora: Jan Oblak (Atletico Madrid)
  Beki Bora: Diego Godin (Atletico Madrid)
  Kiungo Bora: Luka Modric (Real Madrid) 
  Mshambuliaji Bora: Lionel Messi (Barcelona) 
  Mchezaji Mpya: Marco Asensio (Real Madrid*) 
  Mchezaji Bora wa Dunia wa La Liga wa Mwaka: Luis Suarez (Barcelona)
  *Asensio alikuwa kwa mkopo Espanyol 
  NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi ameendelea kufurahua maisha ya soka baada ya kuteuliwa Mshambuliaji Bora wa Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga msimu uliopita.
  Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa, Antoine Griezmann ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa La Liga katika sherehe zilizofanyika leo mjini Valencia.
  Hata hivyo, sherehe hizo ziliingia doa kwa kususiwa na wachezaji Barcelona ambao hawakuhudhuria baada ya kukerwa kwa kitendo cha La Liga kutomuorodhesha kocha wao, Luis Enrique katika tuzo ya Kocha Bora. 
  Enrique hakuwamo hata katika orodha ya wawania tuzo licha ya kuiwezesha Barcelona kutwaa taji la La Liga.
  Nyota wa Real Madrid na Croatia, Luka Modric ameshinda tuzo ya kiungo bora. Mshambuliaji wa Uruguay na Barcelona, Luis Suarez ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora ea Dunia wa La Liga, wakati Atletico Madrid imetoa washindi wa tuzo za kocha Diego Simeone, Jan Oblak kipa bora na Diego Godin beki bora.
  Ajabu mshambuliaji tegemeo wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo wa Ureno hajashinda tuzo yoyote.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ATLETICO MADRID WATAWALA TUZO ZA LA LIGA, BARCA WASUSA...RONALDO APUUZWA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top