• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 31, 2016

  PLUIJM: MTATUUA JAMANI, MECHI TATU WIKI MOJA!

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba si rahisi kucheza mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ndani ya siku nane
  Baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Mbao FC juzi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Yanga watashuka tena dimbani kesho kumenyana na Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, kabla ya Jumamosi kucheza na Prisons hapo hapo Sokoine.
  Ushindo huo uliotokana na mabao ya beki Mtogo, Vincent Bossou, kiungo Mkongo Mbuyu Twite na mshambuliaji Mrundi Amisi Tambwe, unaifanya Yanga ifikishe pointi 27 baada ya kucheza mechi 12 ikiendelea kushika nafasi ya pili, nyuma ya Simba SC yenye pointi 32 za mechi 12 pia. 
  Pluijm amesema kwamba si rahisi kucheza mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ndani ya siku nane

  Na Pluijm amesema leo katika mahojiano maalum na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba pamoja na kwamba vigumu kucheza mechi tatu ndani ya nane, lakini wanataka ushindi kwenye mechi zote za Mbeya. 
   “Tunatakiwa kupambana katika kila mechi. Wapinzani wa Yanga wanacheza kwa bidii ya asilimia 50 zaidi kuliko wanavyocheza na timu nyingine, maana yake kila mechi kwetu ni fainali,”amesema Pluijm.
  Yanga iliondoka Dar es Salaam mapema asubuhi ya leo kwenda Mbeya kwa ndege tayari kwa mechi zake hizo mbili za Jumatano na Jumamosi.
  Mabingwa hao watetezi, wamefikia katika hoteli ya Ifisi Community Centre na baada ya mapumziko jana, leo wanatarajiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Beki wa kulia, Juma Abdul amebaki Dar es Salaam akiendelea na mapumziko sambamba na tiba ya maumivu yake, wakati mshambuliaji Malimi Busungu kwa wiki ya tatu hayupo na timu kwa madai ya matatizo ya kifamilia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PLUIJM: MTATUUA JAMANI, MECHI TATU WIKI MOJA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top