• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 22, 2016

  ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID KUKATA MZIZI WA FITNA LEO USIKU DAR LIVE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  HATIMAYE waimbaji wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali leo Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala.
  Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab.
  Bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.
  Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana leo Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala

  Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitishia mtandao huu kuwa baada ya majigambo mengi kutoka kila pande, leo mzizi wa fitna utakatwa ndani ya Dar Live.
  Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo kamwe Isha hawezi kuyagoka.
  Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID KUKATA MZIZI WA FITNA LEO USIKU DAR LIVE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top