• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 24, 2016

  MANJI AAJIRI MFARANSA KUWA MTENDAJI MKUU YANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imeendelea kujisuka upya baada ya kumuajiri Mfaransa, Jerome Dufourg kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu kwa Mkataba wa miaka mitatu.
  Mfaransa huyo aliyewahi kufanya kazi Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na klabu ya FC Talanta ya Daraja la Pili Kenya anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam wakati wowote kuanza kazi.
  Jerome Dufourg kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu kwa Mkataba wa miaka mitatu

  Kijana huyo wa umri wa miaka 30 atakuwa Dar es Salaam mwezi ujao na ataanza kazi rasmi Novemba 19 baada ya kumalizana na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji.
  Jukumu la kwanza kubwa la Dufourg na kuhakikisha mapato ya klabu yanazidi matumizi. Mwaka jana Yanga iliingiza Sh Bilioni 1.3 wakati ilitumia Sh Bilioni 2.8.
  Tayari Yanga imebadilisha benchi la Ufundi, ikimuondoa aliyekuwa kocha mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm na kumuajiri Mzambia, George Lwandamina.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANJI AAJIRI MFARANSA KUWA MTENDAJI MKUU YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top