• HABARI MPYA

  Friday, October 28, 2016

  RONALDO AREJEA KIKOSINI REAL MADRID IKIIVAA ALAVES KESHO

  NYOTA wa Real Madrid wamerejea mazoezini baada ya kupumzishwa kwenye mchezo wa Kombe la Mfalme, maarufu kama Copa del Rey. 
  Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema wote hawakucheza wakati Real Madrid inashinda 7-1 dhidi ya Cultural Leonesa, lakini wanatarajiwa kurejea kwenye mchezo na Alaves.
  Cristiano Ronaldo amerejea kikosini Real Madrid baada ya kupumzishwa kwenye mchezo wa Copa del Rey

  MABAO 20 YA REAL MADRID KWENYE MECHI NNE ZILIZOPITA 

  Ilishinda 7-1 dhidi ya Cultural Leonesa 
  Ilishinda 2-1 dhidi ya Athletic Bilbao
  Ilishinda 5-1 dhidi ya Legia Warsaw
  Ilishinda 6-1 dhidi ya Real Betis   
  Timu ya kocha Mfaransa, Zinedine Zidane kwa sasa inaongoza La Liga, ikiwazidi Sevilla kwa pointi moja na wakiwa wenye kujiamini, kesho wanamenyana na wenyeji Alaves Uwanja wa Mendizorrotza ambao kwa sasa wanashika nafasi ya13 kwenye msimamo wa La Liga. 
  Zidane anatumaini kwamba hata bila wakali wake hao anaweza akaendeleza utamaduni wa ushindi mnono dhidi ya wapinzani. Katika ushindi mnono dhidi ya Leonesa, wote Alavaro Morata na Marcos Asensio walifunga mabao mawili kila mmoja wakionyesha kwamba wanastahiloi nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza. 
  Baada ya ushindi huo mnono, Real ikiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele, lakini watakuwa na mchezo wa marudiano.
  Alaves watahitaji kucheza vizuri katika safu yao ya ulinzi wikiendi hii, dhidi ya Real Madrid yenye safu kali ya ushambuliaji iliyovuna mabao 20 kwenye mechi zao nne zilizopita. 
  Kukosekana kwa Luka Modric, Casemiro, Sergio Ramos na Dani Carvajal kumempunguzia vitu vjchache mno kocha Zidane katika kikosi chake.
  Real imekuwa ikifunga angalau mabao matano katika kila mechi kwenye mechi zao tano zilizopita na dhidi ya Alaves wanatarajiwa kuendeleza rekodi hiyo kedho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AREJEA KIKOSINI REAL MADRID IKIIVAA ALAVES KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top