• HABARI MPYA

    Saturday, October 22, 2016

    MAHAKAMA YAZUIA MKUTANO YANGA KESHO, MANJI ANAUNGURUMA LEO DAR

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MKUTANO Mkuu wa dharula wa klabu ya Yanga uliokuwa ufanyike kesho umezuiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kufutia kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.
    Kwa mujibu wa hati ya agizo halali la Mahakama, uongozi wa Yanga umezuiwa kufanya Mkutano huo baada ya kesi iliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji na Kampuni ya Yanga Yetu.
    Manji anatarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari leo mchana kutolea ufafanuzi hilo.
    Yanga ilipanga kuwa na Mkutano wa dharula kesho Uwanja wa Kaunda, uliopo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam. 
    Ajenda kuu ya Mkutano huo ni kupitisha Baraza la Wadhamini la klabu hiyo pamoja na kuondoa Mjumbe mmoja na kuweka mpya.
    Na hayo yanafuatia Baraza la Wadhamini kuikodisha timu kwa kampuni ya Yanga Yetu kwa miaka 10, baada ya wanachama kuafiki ombi la Mwenyekiti wao, Yussuf Manji katika Mkutano wa Agosti 6, mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAHAKAMA YAZUIA MKUTANO YANGA KESHO, MANJI ANAUNGURUMA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top