• HABARI MPYA

  Sunday, October 23, 2016

  SAMATTA AISAIDIA GENK KUSHINDA MECHI YA MAHASIMU, AGONGA 90 ZOTE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo amecheza dakika zote 90 na ushei timu yake, KRC Genk ikishinda 1-0 dhidi ya mahasimu wao, Sint-Truiden katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, Uwanja wa Laminus Arena.
  Mechi hiyo ilikaribia kumalizika kwa sare ya 0-0 kama si mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis kufunga bao pekee la ushindi dakika ya 88. 
  Samatta (kushoto) akipiga mpira mbele ya mchezaji wa Sint-Truiden Uwanja wa Laminus Arena leo

  Huo unakuwa mchezo wa 29 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 10 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.

  Katika mechi hizo, ni 15 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na nne msimu huu, wakati 13 alitokea benchi nane msimu uliopita na 10 msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AISAIDIA GENK KUSHINDA MECHI YA MAHASIMU, AGONGA 90 ZOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top