• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 24, 2016

  PLUIJM NA MWAMBUSI SAFARI IMEIVA YANGA, LWANDAMINA KAWASILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABADILIKO ya benchi la Ufundi la Yanga SC yameiva kufuatia kuwasili kwa kocha Mzambia, George Lwandamina jana tayari kusaini Mkataba.
  Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi na Wasaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo wataondoka.
  Na Mzambia, George Lwandamina atakuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.  
  Kocha Mzambia, George Lwandamina anatakiwa kuchukua nafasi ya Pluij Yanga 

  Pluijm amejikuta katika wakati mgumu baada ya Yanga kuambulia pointi 21 kati ya 30 za mechi 10 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Yanga SC imetoa sare tatu, imefungwa mechi moja na kushinda sita tangu kuanza kwa Ligi Kuu – hiyo ikiwa ni mbali na kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Azam kwa penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2.
  Na baada ya mchezo wa Oktoba 1, wakilazimishwa sare ya 1-1 na mahasimu, Simba SC waliokuwa pungufu kwa sehemu kubwa kufuatia Nahodha wao, Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29, baadhi ya viongozi wa Yanga wamependekeza mwalimu huyo aondolewe.
  Lakini habari zinasema Pluijm atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika mabadiliko haya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PLUIJM NA MWAMBUSI SAFARI IMEIVA YANGA, LWANDAMINA KAWASILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top