• HABARI MPYA

    Sunday, October 30, 2016

    MAZEMBE WAIHOFIA BEJAIA SHIRIKISHO

    KOCHA wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Hubert Velud hakubaliani na timu yake kupewa nafasi kubwa ya kuwafunga Mouloudia Olympique Bejaia katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Fainali ya kwanza ya Daudi na Goliath ilifanyika jana Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida na timu hizo zikatoka sare ya 1-1 na sasa mchezo wa marudiano utafuatia Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi, DRC.
    Mzaliwa wa Ufaransa, Velud hakubali kwamba Mazembe kushinda mataji tisa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Bejaia kuwa wanawania taji lao la kwanza mwaka huu kuna nafasi yoyote katika mchuano wao.
    Utabiri wake unatokana na mechi mbili za awali za Kundi A zilizowakutanisha na Bejaia, ya kwanza ikimaliza kwa sare ya bila mabao na ya pili Mazembe wakishinda kwa mbinde 1-0 nyumbani, bao pekee la Rainford Kalaba.
    "Fainali ni mchuano wa 50-50," amesema kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa na klabu za Algeria na kuongeza. 
    “Mouloudia wamethibitisha ubora wao, na sishangai wamefuzu kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho,".
    Mazembe, ambayo mataji yae tisa ya CAF iliyoshinda ni pamoja na Ligi ya Mabingwa, kikosi chake kinaundwa na nyota kutoka nchi tofauti barani Afrika zikiwemo DRC, Ghana, Ivory Coast, Mali na Zambia. 
    Miongoni mwao ni mchawi wa chenga wa Zambia na Nahodha, winga Kalaba, ambaye msimu huu amefunga mabao sita katika Kombe la Shirikisho, hivyo kuongoza kwa ufungaji kwa pamoja na Arsenio 'Love' Cabungula, ambaye klabu yake ya Angola ilitolewa katika mchujo.
    Kocha wa Bejaia na beki wa zamani wa Algeria, Nacer Sandjak amesema amefurahi kukutana na washindi wa pili wa mwaka 2013, Mazembe kuliko mabingwa wa 2015, Etoile Sahel kwenye fainali.   
    “Ikiwa ningetakiwa kuchagua baina ya timu hizo mbili, ningechagua kucheza na klabu ya Kongo kwa sababu Watunisia ni wagumu kukabiliana nao,” alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAZEMBE WAIHOFIA BEJAIA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top