• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 22, 2016

  AZAM YAFUTA MKOSI, YAICHAPA 1-0 JKT RUVU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imefuta mkosi leo baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Shukrani kwake Nahodha wa timu, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 57 kwa mkwaju wa penalti kufuatia beki wa Ruvu kuunawa mpira kwenye boksi.
  Huo unakuwa ushindi wa kwanza kwa Azam FC baada ya mechi sita mfululizo bila ushindi.
  Mechi sita zilizopita Azam ililazimishwa sare ya 1-1 Jumamosi na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, ilifungwa 1-0 na Simba Septemba 17, 2-1 na Ndanda FC mjini Mtwara Septemba 24, sare ya 2-2 na Ruvu Shooting Chamazi Oktoba 2, kabla ya kufungwa 1-0 na Stand United mjini Shinyanga Oktoba 12 na sare ya 0-0 na Yanga Oktoba 16 Dar es Salaam. 
  Refa Ludovic Charles kutoka Tabora alimtoa kwa kadi nyekundu kiungo wa Azam FC, Himid Mao dakika ya 84 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kwa lugha chafu iliyounganishwa na kadi ya kwanza ya kucheza rafu.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Daniel Amoah, Agrey Moris, Ramadhani Singano ‘Messi’/Ya Thomas Renaldo dk80, Himid Mao, Gadiel Maiko, John Bocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Bruce Kangwa/Khamis Mcha ‘Vialli’dk69 na Francisco Zekumbawira.  JKT Ruvu: Said Kipao, Omary Kindamba, Salim Gilla, Hassan Dilunga, Nurdin Mohammed, Rahim Juma, Ismail Amour, Kassim Kisengo/Samuel Kamuntu dk 66, Naftal Nashon/Khamis Thabit, Atupele Green na Pera Mavuo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM YAFUTA MKOSI, YAICHAPA 1-0 JKT RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top