• HABARI MPYA

  Wednesday, October 26, 2016

  YANGA BILA PLUIJM ITAVUNA NINI KWA JKT RUVU LEO?

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC inashuka Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo kumenyana na JKT Ruvu katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Yanga watashuka uwanjani siku moja baada ya kumpoteza kocha wao, Mholanzi Hans Van der Pluijm aliyejiuzulu juzi baada ya takriban miaka miwili ya kuwa kazini tangu Januari mwaka jana.
  Aliyekuwa kocha Msaidizi, Juma Mwambusi ataiongoza timu baada ya kuondoka kwa Pluijm, ingawa tayari taarifa zinasema kuna mabadliko ya benchi zima la Ufundi la Yanga yanafuatia.
  Mzambia George Lwandamina aliwasili juzi Dar es Salaam na inadaiwa amekuja kusaini Mkataba wa kuchukua nafasi ya Pluijm, jambo ambalo limemkera Mholanzi huyo na kuamua kuondoka.
  Pluijm alisema Yanga imemvunjia heshima kwa kumletea kocha mpya bila kumtaarifu na hawezi tena kuendelea kufanya nao kazi. “Nimejiuzulu na sitafanya kazi tena Yanga. Ninafuatilia haki zangu na baada ya hapo nitaondoka,”alisema. Zaidi Pluijm
  Aidha, kuhusu uwezekano wa Mkurugenzi wa Ufundi, Pluijm alisema; “Sipendelei sana hiyo kazi. Nataka kufanya kazi na wachezaji kila siku kwa matakwa ya moyo wangu. Ninaondka, mimi ni kocha mkubwa na wasifu mzuri. Nitapata timu,”alisema.
  Pluijm anaondoka baada ya kuipa Yanga ushindi wa rekodi wa msimu wa 6-2 dhidi ya Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.⁠
  Kwa ujumla, Yanga inapindua benchi zima la Ufundi, ikiwaondoa Pluijm na Wasaidizi wake wote, Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kumpa nafasi Mzambia, George Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.  
  Yanga ambao ndiyo mabingwa watetezi, wanashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu kwa pointi zao 21 za mechi 10, nyuma ya Simba SC wenye pointi 29 za mechi 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA BILA PLUIJM ITAVUNA NINI KWA JKT RUVU LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top