• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 29, 2016

  SIMBA SC KUENDELEZA UBABE LIGI KUU LEO?

  Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
  VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC wanashuka Uwanja wa Kambarage, Shinyanga leo kumenyana na wenyeji, Mwadui FC.
  Kwa ujumla Ligi Kuu inaendelea tena leo na mbali na Mwadui na Simba, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza Toto Africans wataikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, African Lyon watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na JKT Ruvu wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Mabingwa watetezi, Yanga SC watakamilisha mzunguko huu kwa kumenyana na Mbao FC kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Stand United Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Simba ndiyo inaoongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 29 za mechi 11, ikifuatiwa na wenye taji lao, Yanga SC wenye pointi 24 za mechi 11 pia, wakati Stand United yenye pointi 21 za mechi 12 ni ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUENDELEZA UBABE LIGI KUU LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top