• HABARI MPYA

    Monday, March 14, 2016

    YANGA NA AL AHLY HIYOOOOOOOO!

    MATOKEO MECHI ZA KWANZA RAUNDI YA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
    Jumamosi Machi12, 2016
    Sundowns (Afrika Kusini) 2-0 AC Leopards (Kongo)
    Stade Malien (Mali) 2-0 Coton Sport (Cameroon)
    Zesco United (Zambia) 4-1 Horoya (Guinea)
    APR (Rwanda) 1-2 Yanga SC (Tanzania)
    Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) 0-1 ASEC Mimosas (Ivory Coast)
    Club Africain (Tunisia) 1-0 MO Bejaia (Algeria)
    Wydad (Morocco) 5-1 CNaPS (Madagascar)
    Ahly Tripoli (Libya) 1-0 El Hilal (Sudan)
    Recreativo do Libolo (Angola) 0-0 Ahly (Misri)
    Jumapili, Machi 13, 2016
    AS Vita (DRC) 1-0 Ferroviaro (Msumbiji)
    Warri Wolves (Nigeria) 0-1 El Merreikh (Sudan)
    Etoile du Congo (Kongo) 1-1 ES Setif (Algeria)
    St George (Ethiopia) 2-2 TP Mazembe (DRC)
    Enyimba (Nigeria) 5-1 Vital’O (Burundi)
    OC Khouribga (Morocco) 1-1 Etoile du Sahel (Tunisia)
    Union Douala (Cameroon) 0-1 Zamalek (Misri)
    Yanga inaweza kukutana tena na Al Ahly mwezi ujao katika Ligi ya Mabingwa Afrika

    MECHI kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri. Hiyo inafuatia timu zote mbili kuanza vyema katika mechi zao za kwanza, tena ugenini Raundi ya Kwanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki.
    Wakati Yanga iliifunga APR 2-1 mjini Kigali Jumamosi, siku hiyo hiyo Al Ahly nayo ililazimisha sare ya 0-0 na Recreativo do Libolo nchini Angola.
    Wakati Ahly sasa watahitaji ushindi wowote mwembamba kwenye mchezo wa marudiano mwishoni mwa wiki hii mjini Cairo, Yanga hata sare itawasogeza hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kuingia kwenye makundi.
    Yanga na Al Ahly ni timu zenye kufahamiana sana zikiwa na historia ya kukutana mara kwa mara kwenye michuano ya CAF.
    Mara ya mwisho zilikutana mwaka 2014 katika Raundi ya Kwanza na Yanga ikatolewa kwa penalti 4-3, baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA AL AHLY HIYOOOOOOOO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top