• HABARI MPYA

    Thursday, March 03, 2016

    FAYERNOOD YAKUBALI KUISAIDIA FERWAFA KUENDELEZA SOKA RWANDA

    SHIRIKISHO la Soka Rwanda (FERWAFA) iatsaini mkataba wa muda mredu na klabu ya Feyenoord ya Uholanzi kwa ajili ya maendeleo ya soka Rwanda.
    Rais wa FERWAFA, Vincent Degaule Nzamwita amekutaka na Meneja Uhusiano wa Kimataifa wa klabu hiyo, Gido Vader Jumanne kukamilisha mipango kwa ajili ya akademi ya vijana nchini Rwanda.
    Balozi wa Rwanda nchini Uholanzi, Jean Pierre Karabaranga pia alihudhuria mkutano huo, makao makuu ya klabu hiyo mjini Rotterdam.
    “Mkutano ulilenga kuangalia uwezekano kuyafanyia kazi yale ambayo tuliyajadili katika mikutano yetu ya awali na kipi kinahitajika ili kuimarisha uhusiano wetu na Feyenoord,” amesema Nzamwita.

    “Tangu tumepanga kuwa na mashindano ya U-15, msaada wao wa kiufundi utakuwa muhimu sana sana kukuza skka yetu nchini. Tunaamini muda si mrefu tutaanza kunufaika na msaada wao wa kiufundi. Pia tunamhsukuru Balozi Karabaranga kwa msaada wake kuhakikisha kwamba Feyenoord inakuja kusaidia kuendeleza sekta ya soka,” amesema.
    Mwaka jana FERWAFA ilinzisha mashindano ya ligi za vijana chini ya umri wa miaka 15 na miaka 13 (U-15 na U-13) kwa wote, wasichana na wavulana.
    Na mabingwa mara 14 wa Ligi ya Uholanzi, maarufu kama Eredivisie wanasifika kwa kuzalisha wachezaji nyota duniani kama Robin Van Persie ambaye kwa sasa anachezea Fenerbahce ya Uturuki baada ya kuwika Arsenal na Manchester United za Ligi Kuu ya England.
    Wengine ni Giovanni van Brockhorst, Johan Cruyff, Ruud Gullit, Dirk Kuyt, Bruno Martins Indi na Ron Vlaar.
    Akademi ya vijana ya Feyenoord pia ina uhusiano na nchi za Ghana, Nigeria, Afrka Kusini na Vietnam.
    Akademi ya Feyenoord inayojulikana kama Varkenoord, ina mfumo mzuri unaoheshimika nchini Uholanzi ambayo imeshinda tuzo ya Rinus Michels kama akademi bora ya vijana kwa miaka mitano mfululizo tangu mwaka 2009.
    Varkenoord ilitoa wachezaji 11 katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, ambayo ni idadi kubwa kuliko akademi zote duniani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FAYERNOOD YAKUBALI KUISAIDIA FERWAFA KUENDELEZA SOKA RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top