Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
CHAMA cha Soka Dar es Salaam (DRFA) kimefurahia timu tatu za mkoa, Yanga SC, Azam FC na Simba SC wake kumaliza katika nafasi tatu za juu kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyomalizika mwishoni mwa wiki.
Kamati ya utendaji ya DRFA chini ya Mwenyekiti wake, Almasi Kasongo, imesema ni jambo la kufurahisha kuona mkoa wa Dar es Salaam unafanya vizuri kisoka na kuwa mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine.
Timu hizo zimepongezwa kutokana matayarisho waliyoyafanya tangu kuanza kwa msimu, ambapo mabenchi ya ufundi yameonyesha kuwa na nia ya dhati kuleta ushindani katika ligi.
Yanga SC na Azam FC ndizo zitakazoiwakilisha nchi katika michuano ya Afrika mwakani. Yanga itacheza Ligi ya Mabingwa baada ya kuwa bingwa, wakati Azam itashiriki Kombe la Shirikisho baada kumaliza katika nafasi ya pili.
Aidha, DRFA imeipongeza TFF na Kamati ya bodi ya Ligi kwa usimamizi mzuri wa ligi hiyo msimu huu licha ya kuwepo na changamoto ndogondogo kwa vilabu kulalamikia miundombinu ya vyumba vya kubadilishia nguo viwanjani, na uonevu wa baadhi ya waamuzi.
Hata hivyo, DRFA imeishauri TFF kuangalia kwa kina na kuzifanyia kazi changamoto hizo zilizojitokeza msimu huu ili zisijirudie tena katika msimu ujao, kwa lengo la kuiboresha ligi ya Tanzania, ambayo kuanzia msimu ujao itakuwa na jumla ya timu 16.
Pamoja na hayo, DRFA imezishauri Yanga na Azam kujipanga vizuri kwa ajili ya michuano ya Afrika msimu ujao, ili kuandika historia na kuleta mataji hayo kwa mara ya kwanza hapa nyumbani.

![]() |
| Simba SC imemaliza katika nafasi ya tatu Ligi Kuu |

.png)
0 comments:
Post a Comment