KOCHA Pep Guardiola kwa mara nyingine 'amewatolea nje' Manchester City na kuwaambia wazi anataka kubaki Bayern Munich.
Manchester City ambao wamepoteza makali msimu huu kiasi cha kuvuliwa ubingwa wa Ligi Kuu ya England wanamtaka sana Mspanyola huyo ahamie Etihad.
Na mustakabali wa Guardiola kwa sasa The Bavarian hauleweki kutokana na timu hiyo kufungwa mechi nne mfululizo.
Na hali itakuwa mbaya sana kwake iwapo Bayern itashindwa kuitoa Barcelona katika Nusu Fainali ya pili Uwanja wa Allianz Arena Jumanne.
Guardiola amezungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mechi na Barcelona kesho
Baada ya kufungwa mabao 3-0 katika Nusu Fainali ya kwanza Barcelona Mei 6, kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 anatakiwa kushinda 4-0 nchini Ujerumani ili kutinga Fainali.
Lakini alipoulizwa kuhusu ofa ya Manchester City, mchezaji na kocha huyo wa zamani wa Barca, alisemna; "Vijana, nimesema hii mara 200 kwamba nina Mkataba wa mwaka mmoja zaidi hapa. Msimu ujao nitakuwa hapa, ni hivyo tu,".
Guardiola aliiacha timu yake kipenzi Barcelona mwishoni mwa mwaka 2012 baada ya kushinda nayo mataji 14 yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa, kabla ya mwaka uliofuata kujiunga na Bayern na tangu hapo ameiwezesha kushinda taji la Bundesliga mfululizo.


.png)
0 comments:
Post a Comment