ONYESHO la utambulisho wa wasanii wapya wa Mashujaa Band na nyimbo mbili mpya lililofanyika Ijumaa iliyopita, haliwezi kupita hivi hivi bila kuzungumziwa mazuri yake na mabaya yake.
Kama ilivyoandikwa majuzi kupitia Saluti5 ni kwamba onyesho hilo lilifana licha ya mvua kunyesha kwa sehemu kubwa ua usiku huo - Lakini pamoja na kufana kwa onyesho hilo, bado najiuliza ni vipi utawala wa Mashujaa Band ulijivisha miwani ya mbao usoni na na pamba masikioni hadi kuwa na ushujaa wa kendelea na onyesho lile.
Katika muda wote wa onyesho hilo lililoanza saa 3 za usiku pale Mashujaa Grill & Lounge maeneo ya Victoria jijini Dar es Salaam, mvua ilikuwa ikinyesha kwa mwendo wa wastani lakini bila kukatika hata mara moja na kuwalazimu waandaji kuweka matorobali ili kupunguza adha kwa wahudhuriaji walioweza kuwa ‘wabishi’ na kufika ukumbini hapo.
Mvua zile hazikuanza usiku ule wa Ijumaa tu, bali zilianza Jumatano mchana hadi kesho yake, zikaendelea kwa siku nzima ya Alhamisi (usiku na mchana), zikaendelea kutandika kwa mchana wote wa Ijumaa hadi usiku wake.
Maonyesho mengi ya muziki ya Alhamisi na Ijumaa yaliahirishwa, lakini bado Mashujaa wakasema NO, onyesho liko pale pale.
Hali ilikuwa ni mbovu na ndio maana ikaandikwa kuwa: “Ingawa watu hawakuwa wengi ile ya kupitiliza, lakini kwa hali ya mvua iliyokuwepo, Mashujaa Band wamepata cha kujivunia – mtu kutoka nyumbani kwake na kuja kwenye shughuli yako huku mvua inanyesha na huku ukumbi ukiwa ni wa wazi, si jambo la kawaida.”
Kwa hakika mvua zilipunguza ladha za onyesho lile, hata usikivu wa vyombo kwa kiasi fulani uliathiriwa na mvua zilizokuwa zinaendelea, mashabiki hawakuweza kucheza kwa huru kutokana na eneo la kuchezea kutapakaa maji na huku mvua zikiendelea kunyesha.
Hata mahudhurio nayo yaliathiriwa na mvua ile, nina uhakika kusingekuwa na mvua, basi ukumbi ule usingetosha – kumtoa mtu nyumbani kwake na mvua ile kwa dala dala, boda boda au bajaji si jambo la kawaida na ni wazi kuwa Mashujaa waliwakosa watu wanaotegemea usafiri wa aina hiyo.
Onyesho la utambulisho wa nyimbo mpya na wasanii wapya mwanzoni ilikuwa lifanyike mwezi April siku ya Pasaka, nakumbuka Mashujaa walifanya mkutano wa waandishi wa habari kunadi onyesho hilo, lakini halikufanyika.
Mashujaa waliwahi kufanya mkutano wa waandishi wa habari kuhusu kumsajili wako rapa wa FM, Kitokololo na kuweka wazi siku ya kumpandisha jukwaani lakini nalo halikufanyika badala yake ikapigwa show ya kawaida.
Mashujaa wakafanya mkutano na waandishi wa habari kutangaza onyesho la rapa wa DR Congo Bileku Mpasi, lakini onyesho hilo nalo likaota mbaya.
Hiyo inamaanisha kuwa si kila jambo linalotangazwa basi lazima lifanyike hata kama vipo vikwazo visivyozuilika – kuahirisha au kufuta onyesho kwa sababu za msingi si dhambi.
Mvua ile ilikuwa ni sababu tosha ya Mashujaa kuahirisha onyesho lile, inanipa maswali mengi sana kwamba ni kwanini tukio lile lilikuwa ‘haligusiki’. Kulikuwa na siri gani ndani yake? kulikuwa na ulazima gani? Yangetokea madhara gani kama wangeahirisha? Je kulifanya onyesho lile ilikuwa ni kuepuka hasara au kukaribisha hasara?
Kuangalia wanamuziki wakiwajibika jukwaani huku mtu mwingine anakwenda na stuli yake jukwaani na kisha kuanza kusukuma maji kwa fimbo kwenye turubali lililoelemewa na maji ya mvua, ilikuwa ni adha nyingine kwa mtazamaji na hata kwa wanamuziki wenyewe.
Nichukue fursa hii kuwapa pongezi Mashujaa Band kwa kufanya onyesho lile na kupata walichokipata lakini nawaomba wasirudie tena, kumbi za wazi na mvua ni sawa na polisi na kibaka.

.png)
0 comments:
Post a Comment