• HABARI MPYA

    Saturday, May 02, 2015

    BARCELONA WATANGAZA RASMI KUITAKA SAINI YA POGBA

    MKURUGENZI wa Usajili wa Barcelona, Ariedo Braida amethibitisha klabu hiyo ina dhamira ya kumsajili kiungo wa Juventus, Paul Pogba, na kwamba tayari vigogo hao wa Katalunya wameanza mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa timu hiyo ya Serie A, Giuseppe Marotta.
    Tangu aondoke Manchester United, ambako alikuwa hapati nafasi kikosi cha kwanza mwaka 2012, Pogba amekuwa mchezaji gumzo duniani kiasi cha 'kuzitoa udenda' klabu za Ligi Kuu England, sambamba na vigogo wa Ligue 1, Paris Saint Germain.
    Sasa Barcelona imejitosa kwenye mbio za kuwania saini Pogba, ambaye thamani yake ni Pauni Milioni 60, iwapo ataondoka Juventus, na Braida amesema amefanya mazungumzo na rafiki yake Marotta.
    Paul Pogba joined Juventus in the summer of 2012 from Premier League giants Manchester United 

    "Tunampenda Pogba, tunampenda sana. Lakini hiyo haihitaji kusema. Klabu zote kubwa kama bingwa inamtafuta Pogba," amesema Braida akizungumza na Tuttosport.
    "Marotta ni rafiki yangu na tulizungumza kuhusu mambo mengi. Pia tulimjadili Pogba.
    "Bado mdogo, lakini tayari ameonyesha vitu vikubwa. Itakubwa babu kubwa Barcelona ikimpata huyo mchezaji, anayetamanisha sana," amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCELONA WATANGAZA RASMI KUITAKA SAINI YA POGBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top