• HABARI MPYA

    Friday, March 06, 2015

    NKONGO KUCHEZESHA ZESCO Vs AS KALOUM

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    REFA mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Israel Mjuni Nkongo amechaguliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) kati ya wenyeji Zesco FC ya Zambia dhidi ya AS Kaloum ya Guinea.
    Katika mchezo huo wa kwanza wa mzunguko wa pili, Nkongo atasaidiwa na washika kibendera John Kanyenye na Josephat Bulali na mwamuzi wa akiba Waziri Sheha wote kutoka Tanzania, huku Kamisaa wa mchezo akiwa Mayixole Elvin Shishana kutoka nchini Afrika Kusini 
    Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kati ya Machi 13,14 na 15, mwaka huu mjini Ndola, Zambia.
    Israel Nkongo kulia atachezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NKONGO KUCHEZESHA ZESCO Vs AS KALOUM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top