• HABARI MPYA

    Wednesday, March 04, 2015

    MTIBWA SUGAR YAISHUSHA SIMBA SC LIGI KUU

    MTIBWA Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Moro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Ally Shomary dakika ya 52 na Said Mkopi dakika ya 81 na sasa inafikisha pointi 25 baada ya kucheza mechi 17.
    Mtibwa sasa inapanda nafasi ya nne, juu ya Simba SC yenye pointi 22 za mechi 16. Simba SC wanaweza kurudi juu wakiwafunga watani wao wa jadi, Yanga SC Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ndanda FC wamepata ushindi wa ugenini 2-1 dhidi ya wenyeji Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani wakati Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam JKT Ruvu imegawana pointi na Prisons baada ya sare ya 1-1.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAISHUSHA SIMBA SC LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top