KLABU ya Sunderland imetiwa hatiani na Chama Soka England kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake Jumapili wakitoka sare ya 1-1 na Everton Uwanja wa Light.
Wachezaji wa Sunderland waliudhiwa na maamuzi ya refa, Lee Mason kuwapa penalti Toffees dakika ya 76 baada ya Connor Wickham kuangushwa na Seamus Coleman kwenye boksi.
Leighton Baines hakufanya makosa baada ya kwenda kuukwamisha nyavuni mkwaju kufuatia Sebastian Larsson kuwapatia Black Cats bao la kuongoza dakika ya tisa kwa shuti la mpira wa adhabu.
Seamus Coleman akienda chini baada ya kukutana na Connor Wickham kwenye mchezo huo jumapili
Refa Lee Mason akiwasiliana na Msaidizi wake, baada ya tuklio hilo ndani ya eneo la penalti
Wickham na wachezaji wengine wa Sunderland walizozana na refa msaidizi baada ya Everton kupewa penalti
Taarifa ya FA imesema: "Sunderland imetiwa hatiani na FA kufuatia mchezo wao na Everton Novemba 9, 2014. Imeelezwa kwamba katika dakika ya 76 ya mchezo, klabu ilishindwa kuwadhibiti wachezaji wake na klabu imepewa hadi saa 12 jioni ya Novemba 17, 2014 kujibu mashitaka hayo,".
0 comments:
Post a Comment