• HABARI MPYA

    Sunday, November 09, 2014

    STRAIKA SIMBA SC ASHUSHWA TIMU B AKAKUZE KIWANGO

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Ibrahim Hajibu ameshushwa timu ya pili ya Simba SC, baada ya kutomridhisha kocha wa timu ya kwanza, Patrick Phiri.
    Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba ni utaratibu wa kawaida kwa mchezaji aliyepandishwa anapokosa nafasi kikosi cha kwanza anarudishwa kucheza timu ya vijana.
    “Hajibu ni mchezaji aliyesajiliwa kwa ajili ya timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, akapelekwa timu ya kwanza ili kukomazwa. Sasa inapokuwa mchezaji hamridhishi mwalimu wa timu A, basi anarudishwa huku chini ilia apate nafasi ya kucheza,”amesema Kaburu.
    Ibrahim Hajibu kulia akiichezea Simba B leo dhidi ya Ruvu Shooting

    Hajibu leo ameichezea Simba SC katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na akashindwa kuinusuru na kipigo cha 3-2 katika mchezo huo wa utangulizi kabla ya mechi ya wakubwa ya vikosi vya timu hizo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STRAIKA SIMBA SC ASHUSHWA TIMU B AKAKUZE KIWANGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top