• HABARI MPYA

    Tuesday, November 11, 2014

    RONALDO APOKEA TUZO ZA 'UFALME' WAKE LA LIGA NA KUMLILIA DE STEFANO

    MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amemuenzi gwiji wa zamani wa Real Madrid, Alfredo Di Stefano jana wakati akipokea tuzo yake ya ufungaji bora wa mabao katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Hispania.
    “Nataka kutumia fursa hii kusema kwamba ni mbaya sana Don Alfredo Di Stefano hawezi kuwapa hapa kunipa tuzo hii,” Ronaldo alisema mjini Madrid katika usiku wa kupokea tuzo hiyo.
    Gwiji wa Real, Di Stefano alifariki Julai baada ya kupatwa na mshituko wa moyo mjini Madrid akiwa na umri wa miaka 88 na jana Ronaldo pamoja na kupokea tuzo ya Di Stefano, pia alipewa tuzo ya Pichichi kutoka kwa Rais wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo.
    Cristiano Ronaldo akipokea tuzo za Di Stefano na Pichichi kutoka kwa Rais wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo

    Mshambuliaji huyo wa Ureno alifunga mabao 31 katika La Liga akiwa na Real Madrid msimu uliopita ili kushinda tuzo hiyo.
    Katika miaka mitao iliyopita, Ronaldo ameshinda Pichichi mbili, wakati mpinzani wake, Lionel Messi ameshinda tatu. Messi alisinda msimu wa 2009-2010, 2011-2012 na 2012-2013, wakati Ronaldo ameshinda 2010-2011 na 2013-14.
    Aidha, katika miaka mitano iliyopita pia, Ronaldo ameshinda tuzo ya Di Stefano mara tatu na Messi mara mbili. Messi alishinda mara mbili mfululizo 2009-2010 na 2010-2011, kabla ua kumuachia utawala Ronaldo kuanzia msimu wa 2011-2012, 2012-2013 na 2013-2014.
    Mchezaji huyo wa Argentina aliiwezesha Real Madrid kutwaa mataji matao ya Ulaya kuanzia msimu wa 1956-1960. 
    Alichaguliwa Mwanasoka Bora wa Ulaya katika miaka ya 1957 na 1959 na kupewa Urais wa heshima wa Madrid, mwaka 2000.
    Ronaldo amekuwa na mwanzo mzuri msimu huu, akifunga mabao 23 katika mechi 17 za Madrid, huku akitarajiwa kushinda tena tuzo ya FIFA ya Ballon d'Or. Mabao yake 18 aliyofunga kwenye ligi, siyo yanamfanya aongoze kufunga, pia yanaifanya Madrid iwe kileleni mwa La Liga kwa pointi mbili zaidi dhidi ya Barcelona baada ya mechi 11.Cristiano Ronaldo receives the Di Stefano and Pichichi Awards from Atletico Madrid president Enrique Cerezo
    The Portuguese striker's 31 La Liga goals goals for Real Madrid last season earned him the prestigious award
    Together with the Pichichi award Ronaldo holds the Di Stefano trophy awarded to the best player in La Liga
    Ronaldo akiwa ameshika tuzo zake za Pichichi na Di Stefano (kulia) baada ya kukabidhiwa usiku wa jana

    WASHINDI WATANO WALIOPITA WA TUZO YA PICHICHI

    2009-10 Lionel Messi
    2010-11 Cristiano Ronaldo 
    2011-12 Lionel Messi
    2012-13 Lionel Messi
    2013-14 Cristiano Ronaldo 

    WASHINDI WATANO WALIOPITA WA DI STEFANO

    2009-10 Lionel Messi
    2010-11 Lionel Messi
    2011-12 Cristiano Ronaldo
    2012-13 Cristiano Ronaldo
    2013-14 Cristiano Ronaldo  
    “Matumaini nacheza katika ubora wangu, najaribu kurudia mafanikio ya mwaka uliopita,”amesema Ronaldo na kuongeza. “Nina furaha, timu inacheza vizuri na kuimarika. Idadi ya mabao yangu na pasi za mabao nazotoa si mbaya,”. Mechi ijayo, Ronaldo ataichezea Ureno dhidi ya Armenia Ijumaa kufuzu Euro.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO APOKEA TUZO ZA 'UFALME' WAKE LA LIGA NA KUMLILIA DE STEFANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top