MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amekanusha madai kwamba amempa jina la utani ambalo ni tusi Lionel Messi analamuita 'nyuma ya pazia'.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid ametuhumiwa na kumuita kwa nina ambalo ni tusk mpinzani wake huyo wa Barcelona kwenye kitabu cha Guillem Balague, MESSI, lakini Ronaldo amesistiza si kweli.
"Habari zinazosema hivyo ni uzushi na nato a utetezi wanfu juu ya Lionel Messi,"ameandika mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 katika ukurasa wake wa Facebook.
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amekanusha kumuita mpinzani wake wa Barcelona, Lionel Messi kwa nina la 'motherf******' nyuma ya pazia
Nina heshima kubwa kwa wachezaji wenzangu wote, na Messi dhahiri ni hakuna tofauti
"Huu ni bongo kabisa na nimemuhakikishia mwanasheria wangu achukue hatua kwa wahusika.
"Nina heshima kubwa kwa wachezaji wenzangu wote, na Messi dhahiri ni hakuna tofauti,".
Kitabu cha Balague kinazungumzia uhusiano baina ya wawili hao, kikisema si marafiki, lakini wanazuga tu mbele ya jamii kwa maslahi ya vyombo vya habari.
Mwandishi wa habari za soka wa Hispania amesema wachezaji kadhaa Bernabeu wamempa taarifa kwamba, Ronaldo silo tu humuita Messi kwa jina la 'motherf*****' lakini pia yeyote ambaye yuko karibu na mpinzani wake huyo wa Ballon d'Or.
0 comments:
Post a Comment