• HABARI MPYA

    Saturday, November 01, 2014

    RONALDO AFUNGA REAL MADRID IKISHINDA 4-0 LA LIGA NA KUPANDA KILELENI

    REAL Madird imeichapa Granada mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania, maarufu La Liga jioni ya leo Uwanja wa Nuevo Los Carmenes.
    Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo aliifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya pili, kabla ya James Rodriguez kufunga la pili kipindi cha kwanza, Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya 54 na James Rodriguez kukamilisha ushindi huo dakika za mwishoni.
    Ushindi huo, unaifanya Real ipae kileleni mwa La Liga kwa kufikisha pointi 24 baada ya kucheza mechi 10, lakini imecheza mechi moja zaidi dhidi ya Barca, wanaochuana nao kwenye mbio za ubingwa.
    Ronaldo akishangilia na wenzake ushindi wa leo La Liga

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2816966/Granada-0-4-Real-Madrid-Goals-Cristiano-Ronaldo-Karim-Benzema-James-Rodriguez-double-seal-emphatic-away-win.html#ixzz3HqSrJjIj 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO AFUNGA REAL MADRID IKISHINDA 4-0 LA LIGA NA KUPANDA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top