• HABARI MPYA

    Saturday, November 01, 2014

    ARSENAL YAUA 3-0 ENGLAND, SANCHEZ MBILI PEKE YAKE

    ARSENAL imeng’ara katika Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley Uwanja wa Emirates, London.
    Hadi mapumziko hakuna bao lililokuwa limepatikana na iliwachukia hadi robo ya mwisho ya mchezo, The Gunners kuanza kuhesabu mabao yao.
    Alexis Sanchez alifunga bao la kwanza dakika ya 70, kabla ya Callum Chambers kuongeza la pili dakika ya 72 na Sanchez tena kuwainua vitini mashabiki wa Arsenal dakika ya 90.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Arteta/Ramsey dk63, Flamini, Oxlade-Chamberlain/Walcott dk80, Cazorla, Sanchez na Welbeck/Podolski dk80.
    Burnley; Heaton, Trippier, Duff, Shackell, Ward, Arfield 6, Jones, Marney/Chalobah dk80, Boyd, Ings na Sordell/Jutkiewicz dk67.
    Alexis Sanchez ameifungia mabao mawili Arsenal ikishinda 3-0

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2816994/Arsenal-3-0-Burnley-Alexis-Sanchez-Calum-Chambers-break-stubborn-Clarets-resistance-two-minute-second-half-double.html#ixzz3HqPyj9X3 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAUA 3-0 ENGLAND, SANCHEZ MBILI PEKE YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top