• HABARI MPYA

    Monday, November 03, 2014

    MWAKIBINGA ATIMULIWA ‘KIAINA’ BODI YA LIGI, NOOIJ KUTAJA KIKOSI CHA STARS KUIVAA SWAZILAND

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    OFISA Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga amemaliza mkataba wake tangu Oktoba 31 mwaka huu.
    Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na TPLB wanamshukuru Mwakibinga kwa mchango wake kwa kipindi ambacho ameitumikia Bodi, na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya huko aendako.
    TPLB hivi sasa iko katika mchakato wa kupata Ofisa Mtendaji Mkuu mpya kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mwakibinga baada ya muda wa mkataba wake kumalizika.
    Silas Mwakibinga kulia hajapewa Mkataba mpya Bodi ya Ligi
    Wakati huo huo: Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.
    Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.
    Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWAKIBINGA ATIMULIWA ‘KIAINA’ BODI YA LIGI, NOOIJ KUTAJA KIKOSI CHA STARS KUIVAA SWAZILAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top