• HABARI MPYA

    Monday, November 03, 2014

    MEXIME: KAGERA KUIFUNGA YANGA KIMPANGO WAO, SISI TUNAJUA TUNACHEZA NA WAO TU

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime amesema kwamba hatiwshi na ushindi wa Kagera Sugar dhidi ya Yanga SC kuelekea mchezo baina ya timu hizo za viwanda vya sukari Jumamosi.
    Kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime
    Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar Jumamosi Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mexime ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu leo kutoka Manungu kwamba, anatarajia mchezo huo utakuwa mgumu, kaka ambavyo imekuwa mechi zote walizocheza hadi sasa.
    Kagera iliifunga Yanga 1-0 Jumamosi mjini Bukoba, wakati Mtibwa ililazimishwa sare ya 1-1 Morogoro na Simba.
    “Mimi siangalii (Kagera) katoka kumfunga nani, mimi naangalia nacheza na Kagera, najiandaa kucheza na Kagera,”amesema na kuongeza Mexime.
    “Mechi zote za Ligi Kuu msimu huu ni ngumu, hata mechi yetu na Kagera ni ngumu, sisi tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo huo,”amesema Nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars.
    Mexime amesema anashukuru hana majeruhi kikosini kuekelea mchezo huo na katika programu yake, wanafanya mazoezi mara moja kwa siku, jioni pekee, ili asiwachoshe wachezaji.
    Mecky aliyeshinda mataji ya Ligi Kuu mfululizo na Mtibwa Sugar 1999 na 2000 kama mchezaji, ameifanya timu hiyo iongoze lihi hiyo hadi sasa kama kocha, ikiwa pointi 14, nne zaidi dhidi ya Yanga SC na Azam wanaofuatia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MEXIME: KAGERA KUIFUNGA YANGA KIMPANGO WAO, SISI TUNAJUA TUNACHEZA NA WAO TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top