WIKI hii, kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ametaja kikosi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Swaziland na wengi wamevutiwa na kuitwa kwa mkongwe aliyewahi kuchezea Yanga SC, Abubakar Twaha Mtiro.
Mtiro alianza kuchezea Stars mwaka 2000 kama mshambuliaji, baadaye klabu yake ya wakati huo, Yanga SC ikaanza kumtumia kama beki wa kushoto na hakuwahi kuitwa timu ya taifa kwa ajili ya nafasi hiyo- hii ni mara ya kwanza.
Aliachwa Yanga mwaka 2009 na kuna wakati alipumzika soka kabla ya kurudi uwanjani miaka miwili iliyopita msimu huu, akijiunga na Kagera Sugar ya Bukoba.
Lakini binafsi katika kikosi cha Nooij nilisikitishwa na kwamba hakuna mshambuliaji hata mmoja mzalendo anayecheza Ligi Kuu Kuu ya Vodacom Tanzania Bara aliyeitwa katika kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Novemba 16, mwaka huu jijini Mbabane.
Kwenye kikosi hicho kinachoingia kambini kesho Saa 6:00 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, kabla ya kuanza mazoezi jioni yake kwenye Uwanja wa Gymkhana, Nooij amechukua washambuliaji wanaocheza nje watupu.
Hao ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC na Juma Luizio wa ZESCO United ya Zambia.
Mrisho Ngasa na Simon Msuva wote wa Yanga wametajwa kama washambuliaji, lakini sote tunajua kwamba hawa ni viungo wa pembeni, ambao mara nyingine wamekuwa wakitumika kama washambuliaji.
Lakini ukweli ni kwamba, hata katika klabu zao kwa sasa hawachezi nafasi hiyo ambayo Nooij kawaitia Stars- hivyo ukweli unabaki pale pale kwamba, kikosi cha Stars kina washambuliaji wanaocheza nje watupu.
Na ukirejea kwenye Ligi Kuu inayoendelea hivi sasa, chipukizi Mzanzibari, Ame Ally wa Mtibwa Sugar ndiye mshambuliaji pekee mzalendo, ambaye unaweza kusema kidogo anafanya vizuri.
Timu kubwa tatu zinazotegemewa kutoa wachezaji wa Taifa Stars, Azam FC, Simba na Yanga SC safu zake za ushambuliaji zinategemea wacheaji wa kigeni.
Angalau kidogo Patrick Phiri kwa sasa pale Simba SC analazimisha Elius Maguri acheze, lakini haiko hivyo kwa Joseph Marius Omog wa Azam na Marcio Maximo wa Yanga.
Huwezi kumlazimisha mwalimu kupanga mchezaji ambaye anaona hatamsaidia katika kampeni zake za ushindi, lakini tujiulize kama inafikia kikosi cha Taifa Stars kinatajwa na hakuna mshambuliaji hata mmoja anayecheza Ligi Kuu yetu, je tunaelekea wapi?

0 comments:
Post a Comment