KIPA wa zamani wa England, David James amelazimika kuweka mnadani jezi, bukta na mipira aliyoisaini baada ya kuwekwa wazi Mei mwaka huu kwamba amefilisika.
James, ambaye hivi karibuni amekatisha ustaafu wake na kuwa kocha mchezaji wa timu ya Ligi Kuu ya India, Kerala Blasters FC, amejikuta mufilisi baada ya kuachana na mkewe mwaka 2005.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 44, who amechezwa timu kadhaa Ligi Kuu England kama Liverpool, Manchester City na Portsmouth enzi zake na inaelezwa alivuna kiasi cha Pauni Milioni 20 wakati huo.
James akiinua Kombe la FA alilotwaa akiwa na Portsmouth mwaka 2008
James aliichezea mechi 53 England, ikiwemo za Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini
James ameamua kuuza zagazaga kadhaa kama 150 hive alizotia saini yake kupitia kampuni ya Kent-based auctioneer Hilco.
Jezi ya Frank Lampard iliyosainiwa, nguo ya kudakia ya pinki ya Portsmouth na jezi ya NFL ni miongoni mwa bidhaa 150 zilizotiwa mnadanai na James.
Kipa huyo pia ameweka mnadani jezi aliyopewa na kipa wa Chelsea, Petr Cech mwaka katika fainali ya Kombe la FA mwaka 2010 dhidi ya Portsmouth, jezi ya Uholanzi aliyobadilishana na Edwin van der Sar na jezi ya Michael Owen Namba 10 yenye salamu za 'kila la heri' zilizoandikwa. 
Hilco pia wanauza V-reg ya rangi ya zambarau, Vauxhall Astra ya milango mitatu kama sehemu ya bidhaa za James zilizotiwa sokoni
James amecheza mechi 134 akiwa Portsmouth kati ya 2006 hadi 2010, akishinda nayo Kombe la FA mwaka 2008
0 comments:
Post a Comment