KLABU ya Manchester United imechangisha kiasi cha Pauni 210,000 katika hafla ya hisani ya 15 ya ushirikiano wao na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) iliyoambataa na chakula cha usiku jana.
Katika usiku ambao hisia za Waingereza wengi zilikuwa Madrid na London kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, Louis van Gaal na wachezaji wake walikutana Old Trafford kuchangisha fedha hizo kwa ajili ya shirika hilo la watoto.
Wachezaji wengi wa United walihudhuria sherehe hiyo na wapenzi wao na wake zao na wakapiga nao picha nje ya Uwanja.
Wakati shughuli hiyo, inaendelea Arsenal jana ililazimishwa sare ya 3-3 na Anderlecht Uwanja wa Emirates na Liverpool ikafungwa 1-0 na Real Madrid katika mechi za Ligi ya Mabingwa.
Angel Di Maria na mkewe Jorgelina walikuwepo kwenye sherehe hiyo, wakati kulia ni Tyler Blackett na mpenzi wake, Naomi Thomas
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2821261/Manchester-United-players-wives-help-raise-210-00-charity-Gala-Dinner.html#ixzz3IBAVK4dr
0 comments:
Post a Comment