UHOLANZI imechapwa mabao 3-2 nyumbani Amsterdam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Mexico usiku wa kuamkia leo.
Nyota wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela aliifungia mara mbili Mexico dakika ya nane na 62 akicheza mechi ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka mitatu, wakati bao lingine lilifungwa na mshambuliaji wa Real Madrid, Javier Hernandez ‘Chicharito’ dakika ya 69.
Mabao ya wenyeji, Uholanzi waliopoteza makali chini ya kocha mpya, Guus Hiddink aliyerithi mikoba ya Louis Van Gaal aliyetimkia Man United, yalifungwa na Wesley Sneijder dakika ya 49 na Daley Blind dakika ya 74.
Kikosi cha Uholanzi kilikuwa: Krul, Van Rhijn, Vlaar/De Vrij dk24, Veltman, Willems, Blind, Afellay/Wijnaldum dk68, Sneijder/Fer dk81, Huntelaar, Depay/Promes dk60 na Robben.
Mexico: Ochoa, Aguilar, Reyes, Miguel Herrera/Corona dk61, Alanis, Aldrete, Vazquez/Rodriguez dk89, Hector Herrera/Dominguez dk81, Guardado/Ponce dk87, Vela/Giovani dk76 na Hernandez/Jimenez dk76.
Wesley Sneijder akifumua shut kuifungia Uholanzi dakika ya 49 mjini Amsterdam jana, ikilala 3-2 mbele ya Mexico
Carlos Vela akijiandaa kumzunguka kipa Krul kabla ya kuifungia Mexico katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Uholanzi
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2832125/Holland-2-3-Mexico-Carlos-Vela-scores-double-international-return-Javier-Hernandez-strikes-Dutch-upset.html#ixzz3Iud89ief
0 comments:
Post a Comment