• HABARI MPYA

    Monday, November 10, 2014

    BENDI TATU KUSINDIKIZA UZINDUZI WA ALBAMU YA TARSIS MASELA NOVEMBA 21 DAR

    Na Samira Said, DAR ES SALAAM
    BENDI mbili za muziki wa dansi, Akudo Impact, Mashujaa Music pamoja na kundi la mahiri la muziki wa taarab la Jahazi Modern Classic vitasindikiza uzinduzi wa albamu mpya wa msanii, Tarsis Masela unaotarajiwa kufanyika Novemba 21 kwenye ukumbi wa Ten Lounge jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza jana jijini, Meneja wa mwanamuziki huyo, Ray Matata, alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika na bendi zote tatu zimethibitisha kutoa burudani siku ya uzinduzi huo.
    Matata alisema kuwa wameandaa onyesho ambalo litakuwa ni historia katika muziki wa dansi hapa nchini. Masela alisema kwamba amejiandaa kuwapa mashabiki wa dansi wa Tanzania burudani yenye ubora na lengo lake ni kuonyesha kipaji chake katika sanaa ya muziki.
    “Huu ni mwaka wa saba niko Tanzania, nimejiandaa kuwapa burudani bora mashabiki wa muziki na kuwaachia zawadi ambayo hawataisahau kwenye tasnia ya muziki wa dansi,” alisema Masela. 
    Mwanamuziki Tarsis Masela (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo kuhusu uzinduzi wa albamu yake. kulia ni Meneja wa Akudo, Ramadhani Pesambili na kushoto ni Maxmillan Luhanga,Mkurugenzi wa Masoko wa Mashujaa 

    Aliongeza kuwa albamu yake anayotarajia kuizindua ina jumla ya nyimbo nane na itajulikana kwa jina la Acha Hizo.
    Alizitaja nyimbo zinazounda albamu hiyo kuwa ni pamoja na Tabia Mbaya, Mwiko, Chaguo Langu, Tusiachane, Penzi Langu Limezidi Asali, Vidole Vitatu na Nimevulimia.
    Alieleza kwamba katika albamu hiyo ameshirikisha wasanii wa aina mbalimbali ili kuifanya iwe na ubora kwa kupendwa na wadau wa rika tofauti.
    Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi ya Mashujaa, Maximillian Luhanga, alisema kwamba wamekubali kusindikiza uzinduzi wa albamu hiyo kwa kuheshimu kipaji cha Masela na kutaka kuendelea wasanii wa muziki wa dansi.
    Luhanga alisema kwamba hiyo itaondoka ile dhana ya wasanii wa dansi hawapendani na amewataka wanamuziki wengine kufuata nyayo za msanii huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENDI TATU KUSINDIKIZA UZINDUZI WA ALBAMU YA TARSIS MASELA NOVEMBA 21 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top