Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MAHASIMU wa jadi, katika soka ya Tanzania Simba na Yanga SC watamenyana Oktoba 18, mwaka huu katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na timu zote kwa sasa zipo kwenye maandalizi ya mchezo huo.
Simba SC imeweka kambi mjini Johannesburg, Afrika Kusini wakati Yanga SC ipo Dar es Salaam.
Hata hivyo, timu zote zinakosa wachezaji wake waliopo katika timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga SC waliopo Taifa Stars ni kipa Deogratias Munishi ‘Dida’, mabeki Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan na Charles Edward na washambuliaji Simon Msuva na Mrisho Ngassa.
Wachezaji wa Simba SC walipo Stars ambayo imeweka kambi hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam ni mabeki ni Miraji Adam, Joram Mgeveke, viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo.
Katika mazoezi ya Stars, wachezaji wa Simba na Yanga SC wamekuwa kivutio kikubwa kabla ya Jumatatu kwenda kwenye kambi zao kuungana na wenzao kwa maandalizi ya pambano la Oktoba 18, 2014.
Na kwenye mazoezi ya leo asubuhi, Chanongo amemfunga Dida bao zuri viwanja vya Gymkhana, akiwa mbele kidogo ya katikati ya Uwanja alimtoka mchezaji mmoja na kupata upenyo wa kuachia shuti kali lililomshinda kipa huyo wa Yanga SC na kutinga nyavuni.
Hilo lilitokea katika sehemu ya ‘mechi mazoezi’, lakini hata hivyo bao hilo halikukudumu baada ya Thomas Ulimwengu kuwasawazishia akina Dida kwa penalti akimfunga kipa Aishi Manula baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Ikumbukwe Chanongo ndiye aliyeifungia Simba SC bao katika sare ya 1-1 na Simba SC mchezo wa mwisho timu hizo zilipokutana Mei mwaka huu katika Ligi Kuu, akimfunga Dida wakati bao la wana Jangwani akifunga Simon Msuva.

![]() |
Haroun Chanongo leo amemfunga bao tamu Deo Munishi 'Dida' |

Deo Munishi 'Dida' ametunguliwa bao la aina yake na Chanongo leo |
Na kwenye mazoezi ya leo asubuhi, Chanongo amemfunga Dida bao zuri viwanja vya Gymkhana, akiwa mbele kidogo ya katikati ya Uwanja alimtoka mchezaji mmoja na kupata upenyo wa kuachia shuti kali lililomshinda kipa huyo wa Yanga SC na kutinga nyavuni.
Hilo lilitokea katika sehemu ya ‘mechi mazoezi’, lakini hata hivyo bao hilo halikukudumu baada ya Thomas Ulimwengu kuwasawazishia akina Dida kwa penalti akimfunga kipa Aishi Manula baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Ikumbukwe Chanongo ndiye aliyeifungia Simba SC bao katika sare ya 1-1 na Simba SC mchezo wa mwisho timu hizo zilipokutana Mei mwaka huu katika Ligi Kuu, akimfunga Dida wakati bao la wana Jangwani akifunga Simon Msuva.
0 comments:
Post a Comment