GWIJI wa Arsenal, Thierry Henry anavitoa udenda vigogo vya Ufaransa, Paris Saint-Germain na Monaco kwa mujibu wa taarifa nchini humo kwamba klabu hizo zinamtaka kumng'oa mshambuliaji huyo New York.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 37, ambaye amekuwa akiichezea New York Red Bulls tangu mwaka 2010, atamaliza Mkataba wake na timu hiyo ya MLS mwishoni mwa mwaka na atakuwa tayari kurejea Ulaya Januari.
Tetesi zimetawala kwamba Henry anajiandaa kustaafu, lakini Mshika Bunduki huyo wa zamani anaweza kurudi Arsenal kwa mara ya tatu au gazeti la Le10 Sport limesema Henry anaweza kujiunga na moja ya vigogo vya Ligue 1.
Mkuu wa Idara ya kabumbu wa New York, kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard Houllier, amezungumzia tetesi kwamba Henry anaweza kucheza Ligi Kuu ya Ufaransa.
"Ikiwa bado ana uwezo wa kucheza katika Ligue 1? Ndiyo, hakuna tatizo," Houllier ameliambia Le10 Sport.
"Hadi sasa hakuna uamuzi uliochukuliwa, kwa namna moja au nyingine. Thierry bado hajaamua kuacha soka,"amesema Houllier.
0 comments:
Post a Comment